MLINZI WA MSEMAJI WA IKULU HUSSEIN MOHAMMED ADAIWA KUTEKELEZA MAUAJI.

Maafisa wa DCI wanaendeleza uchunguzi wa kifo cha mtu mmoja aliyepigwa risasi na afisa wa polisi ambaye pia ni mlinzi wa msemaji mkuu wa Ikulu ya Nairobi, Hussein Mohammed.

Kulingana na baadhi ya wananchi walioshuhudia kisa hicho, wamesema kuwa tukio hilo lilichangiwa pakubwa na mzozo kati ya afisa huyo wa polisi kwa jina Mohamed Yusuf Kaynan na Amos Langat ambaye kwa sasa ni marehemu.

Aaron Kipkorir, ambaye ni kakake marehemu amesema kuwa tukio hilo la mnamo siku ya jumapili usiku katika mtaa wa Kawangware kaunti ya Nairobi, lilifanyaka katika eneo la mchezo unaofahamika kama Pull Game huku wananchi wakikashifu vikali suala hilo.

Aidha Kipkorir pamoja na wakaazi wa eneo hilo sasa wanaotoa wito kwa serikali kuwasaidia kupata haki dhidi ya afisa huyo wa ulinzi.