MASHAMBULIZI YA MAGAIDI WA ALSHABAAB YAONGEZEKA KATIKA KAUNTI ZA KASKAZINI MASHIRIKI MWA TAIFA HILI.

Wanamgambo wa Alshabaa wamemuuwa afisa mkuu wa polisi wa akiba katika kaunti ya Mandera, siku moja baada ya magaidi hao kushambulia kambi ya polisi  hao kaunti ya Garissa.

Afisa huyo ambaye pia ni mkuu wa usalama katika afisi ya gavana wa kaunti hiyo ya Mandera, Mohammed Adan Khalif, alikumbana na mauti yake baada ya magaidi hao kuvamia makaazi yake.

Gavana wa kaunti hiyo ya Mandera, amewanyooshea kidole cha lawama maafisa wa polisi kaunti hiyo, kwa madai ya kupuuza taarifa za ujasusi ambazo awali zilikuwa zimesambazwa katika eneo hilo.

Gavana huyo amelalamikia suala la hatua za dharura za kiusalama, kutochukuliwa na maafisa hao licha ya kupokea taarifa hizo huku akisema kuwa kwa sasa jukumu kuu la maafisa hao, imekuwa kuchukua miili baada ya wananchi kuuwawa na wanamgambo hao na sio kuwalinda.