‘MLIMA UNAWENYEWE’ ASEMA GAVANA WA KAUNTI YA NYERI MUTAHI KAHIGA.

Huku rais William Ruto akiendeleza ziara yake katika eneo la Mlima Kenya, viongozi wa eneo hilo wamemtaka kiongozi huyo wa taifa, kufahamu kuwa sio kiongozi mkuu wa siasa za eneo hilo, la Mlima.

Wakiongozwa na gavana wa kaunti ya Nyeri, Mutahi Kahiga amesema hatua ya Ruto kuwa kiongozi wa taifa na kuanzisha miradi eneo hilo, ndiyo sababu kuu za viongozi hao kumkaribisha katika kaunti hiyo na eneo la Mlima Kenya kwa jumla.

Akizungumza na waandishi wa habari, Kahiga amesema kumekuwa na utofauti mkubwa wa mihemko ya kumkaribisha kiongozi wataifa, hasa katika kaunti hiyo ya Nyeri, kufuatia tofauti zilizo ibuka kati yake baadhi ya viongozi wa Mlima Kenya, wakiongozwa na aliyekuwa naibu wa rais Rigathi Gachagwa.