WAZAZI WATAKIWA KUCHUNGUZA IWAPO WANAO WANAUGUA USONJI.

Wazazi nchini wametakiwa kuwapeleka wanao kwenye hospitali na vituo vya afya vilivyo karibu, ili kufanyiwa vipimo dhidi ya maradhi ya Usonji, iwapo watashuhudia utofauti wa tabia zao kwenye jamii.

Haya ni kwa mujibu wa afisa wa shirika linalo husika na masuala ya watoto kaunti ya Kilifi la Kuhenza, Veronica Kariuki, ambaye amesema kuwa mojawapo ya dalili za mtoto kuuugua maradhi hayo, ni hatua yake kuendeleza hali ya utukutu na usumbufu wa hali ya juu.

Akizungumza na lulu fm amesema kuwa watoto hao pia, hukataa kubebwa kila mara, kula vyakula aina moja, wengine wao wakipenda kunyamaza kwa mda mrefu huku wengine wakisalia katika sehemu moja kwa mda mrefu zaidi.

Afisa huyo amesema kuwa licha ya kutokuwepo kwa matibabu ya maradhi ya Usonji almaarufu Autism, uongojwa huo unaweza kuthibitiwa kwa kumsaidia muathiriwa kuwa na wezo wa kufanya shughuli zake kwa utulivu kama wanadamu wengine, iwapo dalili hizo zitagunduliwa mapema.

Kwa mujibu wa shirika la afya duniani WHO, mtoto mmoja kati ya 25 huugua Usonji yaani Autism hapa nchini Kenya.

Haya yanajiri huku mwezi Aprili ukitengwa ili kuhamasisha umma kuhusiana na maradhi hiyo kitaifa.