Mkurugenzi mkuu wa elimu kaunti ya Tana River Khalif Hassan amesema mikakati thabiti imewekwa na idara usalama kwa ushirikiano na wizara ya elimu kuhakikisha hakuna visa vyovyote vya wizi wa mitihani vinashuhudiwa kutoka kwa watahiniwa wa kidato cha nne KCSE kwenye kaunti hiyo.
Hassan amesema Jumla ya wanafunzi 2,120 wakiwemo wasichana 971 wanatarajiwa kufanya mtihani huo wa kidato cha nne kaunti ya Tana River.
Kulingana na Hassan hakujakuwa kukishuhudiwa visa vya udanganyifu wa mitihani ya kitaifa na kuwa watahakikisha watahiniwa wanalindwa vilivyo dhidi ya visa vyovyote vya utovu wa usalama.
Aidha, amesema idadi ya wanafunzi wanaofanya mtihani wa kitaifa kwenye kaunti ya Tana River iko chini mno.
MIKAKATI YAWEKWA TANA RIVER KUDHIBITI VISA VYA WIZI WA MITIHANI WA KIDATO CHA NNE
