Beki wa zamani wa KCB, wanamvinyo Tusker FC pamoja na Wazito FC Mark Odhiambo ameaga dunia baada ya kuugua kwa muda kutokana na uvimbe katika ubongo wake.
Baada ya kustaafu soka Odhiambo amekuwa akijihusisha na biashara ya uchukuzi kama dereva wa mabasi ya Umoja jijini Nairobi.
Mark Odhiambo alikuwa katika kikosi cha Harambee Stars kilichovaana timu ya taifa ya Nigeria mwaka 2014 katika mashindano ya kungangania tikiti ya kufuzu kwa mashindano ya kombe la dunia.

