Afisa katika shirika la kijamii la KECOSCE kaunti ya Tana River, Steven Otoi amelitaka jopo la kuskiza na kuchukua mapendekezo ya mwananchi ya mipangilio ya serikali ya kaunti ya miaka mitano CIDP kuhakikisha inatekeleza mapendekezo ambayo yalitolewa kwenye vikao vya kukusanya maoni ya umma.
Otoi amesema serikali ya kaunti imekua na tabia ya kutekeleza miradi ambayo haikupendekezwa na Wananchi akisema huo ni ukiukaji mkubwa wa sharia.
Amesema ni lazima mapendekezo yanayotolewa na Wakenya yatekelezwe kwa manufaa yao kwani hao ndio ambao wanajua miradi ambay ni muhimu kwao na itakayowanufaisha.
Aidha amependekeza kujengwa kwa hifadhi ya watoto wanaodhulumiwa kwenye jamii ili kufanikisha utatuzi wa visa visa hivyo ili wanaohusika wakabiliwe kisheria.
JOPO LA KUSKIZA NA KUCHUKUA MAONI KAUNTI YA TANA RIVER LATAKIWA KUTEKELEZA MAPENDEKEZO YANAYOTOLEWA NA WENYEJI

