Ni afueni kwa Hospitali za kaunti ya Kilifi baada ya Serikali ya kaunti ya Kilifi kupokea vifaa zaidi vya matibabu kutoka kwa serikali ya Hungary.
Akizungumza baada ya kutoa ufadhili wa vifaa hivyo, Balozi wa Hungary Nchini Kenya Zsolt Meszaros amesema vifaa hivyo vimegharimu takriban shillingi millioni tano na vitsaidia zaidi katika sekta ya maabara kwa uchunguzi wa magonjwa mbalimbali.
Aidha Zsolt amebainisha kuwa serikali ya Hungary inalenga kutoa ufadhili wa masomo kwa baadhi ya wanafunzi katika kaunti hiyo.
Kwa upande wake, Gavana wa kaunti ya Kilifi Gideon Mungaro amesema serikali ya Hungary imeahidi kuleta vifaa zaidi hivi karibuni na kuwa baada ya serikali kusambaza madawa kwa takriban vituo 150 vya afya kaunti hiyo, sasa wanalenga kuboresha huduma za afya kwa kuhakikisha vifaa vya kisasa vya afya vinapatikana Hospitalini.
HOSPITALI ZA KAUNTI YA KILIFI ZAPOKEA VIFAA VYA MATIBABU

