Hatimaye mTimu ya taifa ya Harambee stars itaweza kuzicheza mechi zao za nyumbani mbele ya mashabiki wao, hii ni baada ya Uwanja Wa Nyayo kufungua Milango Yake tayari Kua mwenyeji WA mechi ya kuhuzu kwa kombe la Dunia mwaka WA 2026 dhidi ya Gabon tarehe 24 Machi.
Kufuatia viwanja duni Kenya ililazimika kucheza mechi zake za nyumbani ugenini, ikicheza mechi ya nyumbani mwisho tarehe 12 September mwaka juzi dhidi ya Sudan Kusini.
Viwanja vya Moi na kasarani pia vitatumika kuandaa michuano ya Chan na Ile ya Afcon ya mwaka WA 2027
Wakati hayo yakijiri huenda Mshambuliaji Wa zamani Wa Gor Mahia na mfungaji Bora Wa ligi kuu hapa nchini Wa msimu uliopita Benson Omalla, akarejea kucheza soka la hapa nchini, kukiwa na madai ya kutaka kusajiliwa na klabu ya ligi kuu hapa nchini Shabana.
Omalla aliachana na Kogalo Agosti Mwaka Jana na kujiunga na klabu ya AL Safari inayoshiriki ligi kuu ya Lebanoni, akipata muda mchache uwanjani kwenye miezi Yake mitano na klabu hio.
Mchezaji huyo Wa Zamani Wa Western Stoma alikua mfungaji Bora Wa ligi kuu hapa nchini kwa msimu mwili ikifuatana, akifunga magoli 26 msimu WA 2022/2023 na magoli 19 msimu WA 2023/2024

