GACHANGWA AWEKA WAZI NANI ATAKAYE KUWA MWENYEKITI WA CHAMA CHAKE.

Aliyekuwa naibu wa rais katika taifa hili Geoffrey Rigathi Gachagwa, ameendeleza kampeni zake dhidi ya rais William Ruto, wakati rais akitarajiwa kufanya ziara katika eneo la mlima kenya wiki ijayo.

Gachangwa ameibua madai ya kuhadaiwa na rais William Ruto, kabla yake kuridhia mwaliko wa kujiunga na muungano wa Kenya kwanza na hata kupewa nafasi ya naibu wa rais.

Akizungumza katika kaunti ya Kajiado, Gachagwa amemsuta Ruto kwa kukosa kutimiza ahadi alizotoa kwa wakenya huku akitoa wito wa amani kudumishwa katika taifa hili.

Aidha, Gachangwa ameahidi kutangaza chama chake kipya mwezi Mei mwaka huu na kuweka wazi kuwa mwenyekiti wa chama hicho, atakuwa kiongozi wa jamii ya Maasai katika kaunti ya Kajiado.