Naibu rais Prof Kithure Kindiki amekagua miradi ya maendeleo inayoendelea katika kaunti ya Murang’a, kabla ya ziara ya rais William Ruto katika eneo hilo juma lijalo.
Akizungumza katika eneo bunge la Mathioya, baada ya kukagua soko la Gikoe, pamoja na mradi wa ujenzi wa nyumba za bei nafuu, amesema kuwa licha ya kila mkenya kuwa na haki ya kuishi maisha bora, gharama ya ujenzi wa nyumba ndiyo, sababu kuu ya wakenya wengi kuishi maisha duni.
Kindiki amesema kuwa hatua hiyo, ndiyo sababu kuu ya serikali ya kitaifa kuanzisha mpango wa ujenzi wa nyumba za bei nafuu katika eneo hilo.
Naibu wa rais vile vile amesema kuwa ziara hiyo ya rais William Ruto, haitakuwa na shughuli za kisiasa, ila juhudi kabambe za kutimiza ahadi zake za kabla ya uchaguzi.