Bingwa wa dunia katika mbio za masafa marefu, Eliud Kipchoge hapo aliweka rekodi mpya baada ya kukamilisha mbio za marathon za kilomita 42 ndani ya masaa 2.01.9 rekodi ambayo anajivunjia yeye mwenyewe rekodi aliyoiweka miaka minne iliyopita.
Kipchoge mwenye umri wa miaka 37 sasa ndio bingwa wa dunia katika mbio za Berlin marathon akipungyuza sekunde 30 muda aliouweka mwaka wa 2018 katika mji mkuu wa Berlin nchini Ujerumani.
Sasa Kipchoge ameshinda mbio 15 za marathon Kati ya 17 alizoshiriki katika maisha yake, zikiwemo mara mbili kwenye olimpiki pamoja na mataji 10 makubwa.
Kichoge alimaliza karibu dakika tano mbele ya Mkenya mwenzake Mark Korir, aliyemaliza katika nafasi ya pili kwa muda wa masaa mawili, dakika tanon na sekunde 58. Muethiopia Tadu Abate alimaliza katika nafasi ya tatu na muda wa masaa mawili dakika sita na sekunde 28.
Kipchoge sasa amejivunia kitita cha shilingi za Kenya milioni 13.7 kwa kuvunja rekodi yake mwenye pamoja na marupurupu mengine yanayotokana na ubingwa aliouhifadhi hapo jana katika mbio hizo za Berlin.

