Dirisha la Uhamisho la kati kati ya Msimu ya Ligi Kuu hapa Nchini, ligi ya NSL na divisheni ya kwanza , Limefunguliwa Rasmi hii leo tarehe thelathini na Moja January hadi tarehe ishirini na Nane Februari, Vilabu vingi Vikipania Kutumia Fursa Hii kuimarisha Vikosi Vyao.
Klabu ya Nyumbani ya Bandari inadhamiria kumrudisha kambini mchezaji wao wa zamani Abdalla Hassan, aliyejiunga na Klabu ya Coastal Union nchini Tanzania tarehe nne Julai mwaka Jana, pamoja na mchezaji mwenza John Mark Makwatta aliyekua akihudumia Kariobangi Sharks hapo Zamani.
Kwa Upande Wao Tusker wako Mbioni kumbakisha mshambuliaji wao Ryan Ogam Ugani Ruaraka, hii ni baada ya vigogo wa Ligi Algeria USM Alger kuziwinda Huduma za Mfungaji huyo bora sasa wa Ligi kuu hapa Nchini, wakidai kulipa ada ya Shilingi milioni tatu nukta Tisa Pesa Taslim za Kenya zilizowekwa na Tusker ili kumpata Ogam.
Mohamed Karisa ambaye ni winga aliyekuwa anakipiga kwenye klabu inayomilikiwa na Mshambuliaji wa timu ya taifa Harambee stars Michael Olunga nazungumzia MOFA sasa amejiunga na Dimba Patriots
Kwa majuma kadhaa sasa Karisa amekuwa akipiga tizi na klabu ya 3k ya kocha Francis Chenge na baadaye kusajiliwa na Dimba Patriots inayoshiriki katika ligi ya daraja la pili kitaifa NSL
Taarifa zaidi zasema kuwa baada ya kuachana na MOFA Karisa alijiunga na Kibera united kabla ya kwenda Dimba Patriots ambako kwa sasa amecheza dakika zake 90 za kwanza katika mechi ya kirafiki dhidi ya Tusker FC ambako Dimba walipoteza kwa mabao 2-0

