Afisa mkuu mtendaji wa wa shirikisho la soka nchini Kenya Barry Otieno amezitaka kaunti kote nchini kushirikiana na matawi ya shirikisho hilo kuboresha ligi.
Akiongea na Tama La spoti kwa njia ya simu Otieno amesema kwamba shirikisho hilo linapania kuanzisha ligi ya vijana wasiozidi umri wa miaka kumi na mitano hivyo kuzitaka kaunti kushirikiana katika uandaaji wa ligi hiyo.
“Shirikisho limezidi kuhakikisha kwamba vijana kote nchini wanapata chance ya kushowcase na kumonetize talents zao. Tumesign na Safaricom Chapa Dimba na tutakuwa tunalaunch in June na hii tournament ambayo itachezwa Kenya nzima na sio tu kwa mpira kuna chance pia ya kupata scholarship za TVET.
“Safaricom watapeana scholarship 100 kwa wachezaji bora katika kila region but tunaomba macounty government zisaidie branches zetu za FKF especially sasa ambapo tunalaunch ligi za youth 13 and 15 years,” Amesema Otieno
Otieno amedokeza kwamba mchakato wa kusaka vipusa wasiozidi umri wa miaka 18 watakaopeperusha bendera ya Kenya katika michuano ya CECAFA unatarajiwa kung’oa nanga Ijumaa.
Kuhusu swala la upangaji wa mechi kwa maana ya match fixing Mkurugeni huyo amesema kwamba shirikisho hilo limesimamisha takriban wanamichezo 25.
“Match fixing is a global issue. Tunaomba tu wachezaji, makocha na football administrators wakuwe on the look out kwa sababu match fixing inaaffect sana integrity ya ligi. Integrity ya ligi ikienda chini then wadhamini kuja kudhamini inakuwa ngumu. So far tumesuspend players, coaches na referees about 25,” alisema Otieno.

