BUNGE LA KAUNTI YA KWALE KUJADI MUSWADA WA KUKABILIANA NA DHULUMA ZA KIJINSIASEXUA

Bunge la kaunti ya Kwale limeanza kujadili muswada unaopania kukabiliana na visa vya dhuluma za kijinsia baada ya kuwasilishwa bungeni humo.

Mwenyekiti wa kamati ya masuala ya kijinsia Rachel Katisya amesema muswada huo unalenga kuwalinda wanawake na watoto dhidi ya dhulma za kijinsia.

Katisya amesema ndani ya mswada huo kuna mapendekezo ya kuitaka serikali kujenga vituo maalum vya kuwaokoa waathiriawa wa dhulma hizo.

Naye mwakilishi wa wadi mteule kwenye bunge hilo, Teresia Muoki amesema watashirikiana ili kuhakikisha mswada huo unapitishwa kuwa sheria katika kipindi cha miezi minne ijayo akisema kuwa utasaidia sana kukabiliana na ongezeko la dhulma katika jamii.