Klabu ya Bumbani Stars ambao walishinda ligi ya daraja la pili kitaifa msimu ulopita ni rasmi sasa imefuzu kushiriki katika ligi ya daraja la kwanza kitaifa msimu ujao.
Hi ni kufuatia matokeo yao katika mashindano ya mini lieage yalofanyika wiknedi hii na hii leo pia.
Kutokana na ushindani mkali timu ilomaliza katika nafasi ya pili msimu uliopita Ziwani Youth ililemewa na kushindwa kufuzu kwa mashindano haya kufuatia matokeo duni kwenye mini league.
Sasa Bumbani Stars na klabu ya Dynamo iloshindanishwa na klabu hiyo ya vijana wa kwale inayoongozwa na kocha mwaduka bakari pia imefuzu kushiriki katika mashindano ya Div one.
Sasa Bumbani stars itakuwa timu ya pili kutoka pwani msimu ujao itakayoshiriki katika mashindano ya daraja la kwanza sawa na Young Bulls ya Malindi baada ya Malindi United kushuka daraja msimu uliopita.

