Askofu mkuu wa kanisa katoliki jimbo la Mombasa Martin Kivuva ameitaka serikali kuu kupitia idara husika kuwekeza zaidi katika miradi ya uchimbaji mabwawa ili kudhibiti baa la njaa na kaingazi nchini.
Akizungumza katika kaunti ya Mombasa Kivuva amesema iwapo hilo litatekelezwa itakuwa afueni kwani hakutakuwa na visa vya watu kukabiliwa na baa la njaa nchini Kenya.
Amesema uchimbaji huo wa mabwawa utawawezesha Wakenya kupata maji na kuendeleza kilimo nyunyizi ili kuhakikisha kuna chakula cha kutosha nchini.
Vilevile, ametoa wito kwa Wakenya kuwa mstari wa mbele katika upanzi wa miti ili kutunza mazingira.
ASKOFU MARTIN KIVUVA AMEITAKA SERIKALI KUU KUWEKEZA ZAIDI KATIKA MIRADI YA UCHIMBAJI WA MABWAWA NCHINI

