Wizara ya kawi nchini imetoa wito kwa wakenya kulinda vifaa vya umeme dhidi ya wezi, ambao hutekeleza uharibifu na kisha baadae kuving’o na kuuza vifaa hivyo.
Katibu katika wizara hiyo Alex Wachira, amesema kuwa uharibifu wa vifaa hivyo, huchangia hasara kubwa kwa serikali katika kufanya marekebisho yake.
Akizungumza katika kaunti ya Murang’a, katibu Wachira amewataka maafisa wa idara ya usalama, kushirikiana na wananchi katika kuwafichua wahalifu wa vifaa vya umeme katika jamii.
Aidha, amewapongeza wananchi wa eneo la Magumu kaunti ya Nyandarua kwa kuwakabili vijana waliokuwa na nia ya kuiba vyuma vilivyo kwenye nyaya za umeme.

