WANAHARAKATI WATILISHAKA HATUA YA SERIKALI KUWALIPA FIDIA WAATHIRIWA WA MAANDAMANO.

Mwanaharakati wa shirika la Vocal Afrika, Hussein Khalid ametilia shaka tangazo la serikali ya kitaifa, kuhusiana na malipo ya fidia kwa waathiri wa maandano humu nchini.

Hussein amesema kuwa serikali kuu, ilikosa kutoa maelezo kamili kuhusiana na waathiriwa wa maandamano yapi, watakao nufaika na fidia hiyo.

Vile vile ameongeza kuwa serikali pia, ilikosa kutoa mwelekeo wa jinsi itakavyo fanikisha shughuli za kuwatambua waathiriwa wa maandamano hayo.

Aidha, ameweka wazi kuwa wanaharakati hao hawapingi suala la waathiriwa wa maandamano kulipwa fidia, ila wanaitaka serikali kuu, kutoa maelezo kamili kuhusiana na suala hilo huku akisisitiza, kukamatwa kwa maafisa waliohasiri waandamanaji.