SERIKALI YA KITAIFA YASEMA VIJANA WENGI WAMENUFAIKA NA FEDHA ZA HAZINA YA HUSLER.

Rais William Ruto amesema kuwa zaidi ya wakenya milioni 26, wamenufaika na mikopo ya hazina ya HUSLER kote nchini.

Kulingana na Rais, milioni tisa kati yao, wamekuwa wakikopa mara kwa mara, hatua ambayo anasema imedhirisha kuwa wakenya wengi wamefaidika pakubwa na hazina hiyo.

Akizungumza katika maadhimisho ya siku ya vijana nchini katika chuo kikuu cha Masinde Muliro kaunti ya Kakamega hii leo, Rais William Ruto amesema hazina hiyo, kufikia sasa imekopesha shilingi bilioni 7 na kupata faida ya shilingi bilioni tano tangia ilipoanzishwa.

Kwa upande wake waziri wa michezo na vijana Salim Mvurya, amempongeza rais Ruto kwa kile alichosema amechangia pakubwa katika kuleta suluhu la matatizo yanayo wakabili vijana.

Naye katibu kwenye idara ya vijana Fikirini Jacobs, amesema watajitahidi kuhakikisha kuwa vijana wengi zaidi, wanapata fursa ya kushiriki meza ya maamuzi katika ngazi tofauti za serikali kuu.