Makaburi mengine saba, mafuvu, na mifupa ya binadamu imepatikana katika kijiji cha Kwa Binzaro kaunti ya Kilifi .
Afisa mkuu wa upelelezi kaunti ya Kilifi Robert Kiinge, amethibitisha matukio hayo huku akihofia kwamba huenda wafuasi wengi wa dhehebu potofu wamefariki katika eneo hilo.
Kiinge amesema kuwa makaburi hayo, niya kina kifupi mno na waathiriwa walizikwa kwa kutumia makaratasi ya lailoni.
Vilevile kiinge amefichua kuwa shughuli ya ufukuzi wa makaburi hayo zitaanza hivi karibuni kama ilivyoagiza mahakama kuu ya Malindi.
Aidha, kiinge ameeleza hofu ya kuwa huenda watoto sita walioripotiwa kupotea kuwa ni miongoni mwa milli iliyozikwa eneo hilo.
Haya yanajiri huku watu 11 wakisalia korokoroni, wakati uchunguzi unapoendelea.

