WIZARA YA USALAMA YASISITIZA GACHAGUA KUANDIKISHA TAARIFA KATIKA AFISI ZA DCI PINDI ATAKAPO REJEA HUMU NCHINI.

“Iwapo aliyekuwa naibu rais Rigathi Gachagua hata andikisha taarifa kwa idara ya polisi, kuhusiana na matamshi yake ya serikali ya taifa hili kushirikiana magaidi, tutahakikisha kuwa anafanyiwa uchunguzi wa afya ya akili yake.”

Ndiyo matamshi ya waziri wa usalama wa ndani Kipchumba Murkomen, ambaye amesema kuwa Gachagua amekuwa akizungumzia masuala tata, ambayo yanaweza kuweka taifa hili pabaya katika ramani ya ulimwengu.

Akizungumza na wanahabari katika kaunti ya Narok, Murkomen ameelezea kuwa idadi kubwa ya wanasiasa, ambao hupoteza nafasi kuuu za uongozi serikalini, hukabiliwa na msongo wa mawazo na hivyo kuna haja ya kiongozi huyo kufanyiwa uchunguzi.

Murkomen amewanyooshea kidole cha lawama wakenya sawa na waandishi wa habari, kwa kusambaza kanda za video ambapo kiongozi huyo, hukashifu serikali kuu akisema kuwa wanamchochea kuzungumza zaidi.