Mshauri wa masuala kisiasa katika afisi ya rais William Ruto, Karisa Nzai amewaonya wakenya dhidi ya kugawanywa kwa misingi ya kisiasa.
Karisa Nzai amesema kuwa siasa za ukabila zinaweza kuchangia katika kushuhudiwa kwa migawanyiko ndani ya taifa hili.
Akizungumza katika kaunti ya Mombasa, amesema kuwa wakenya wanapaswa kudumisha umoja utakao sababisha kushuhudiwa kwa amani katika taifa hili.
Karisa aidha amewataka wananchi kujitenga na wanasiasa wanao endeleza kampeni za uhasama wa kikabila humu nchini.

