Waziri wa Kawi Opiyo wandai amewaonya wafuasi wa ODM kitaifa dhidi ya kupinga serikali ya rais William Ruto.
Wandai amesema kuwa itakuwa vigumu kwa baadhi ya wasiasa kukabiliana na rais Ruto kwenye kipute cha uchaguzi mkuu wa mwaka 2027 kutokana na utendakazi wa baraza lake.
Akizungumza katika kaunti ya Kisii amesema kuwa sasa chama cha ODM kipo ndani ya serikali na hivyo wafuasi wake wanapaswa kutulia na kfurahia matunda ya kuwa ndani ya serikali tawala.
Aidha ameelezea kuwa na imani kuwa huenda rais Ruto akashinda uchaguzi wa mwaka 2027.

