WIZARA YA AFYA YATANGAZA KUPUNGUZWA KWA MISHAHARA YA WANAGENZI.

Marupurupu ya wauguzi wanagenzi na matabibu imepunguzwa kufuatia agizo la mahakama wiki jana.

Katibu katika Wizara ya Afya Mary Muthoni, amesema kuwa wanagenzi wapya watakaoajiriwa watapokea marupurupu yaliyopunguzwa jinsi ilivyoamrishwa na mahakama.

Wanagenzi wapya wa shahada ya digrii, watakuwa wakipokea marupurupu ya kati ya shilingi 27,000 na 35,000, wakati wanagenzi wa Utabibu wakipokea kati ya shilingi 47,000 na 70,000.

Wanagenzi Mafamaisa, watalipwa kati ya shilingi 47,000 na 70,000.

Serikali kwa sasa imewaajiri matabibu wanagenzi 145 wa sahada ya digrii, 1,270 wa stashahah ya utabibu na wauguzi wanagenzi wa stashahada 1,283.

Tume ya kuratibu mishahara, ilitangaza mwezi Machi kuwa wanagenzi watakuwa wakipokea marupurupu yasiyozidi shilingi 25 ,000 kwa mwezi.