Chama cha Jubilee kimejiunga na viongozi wengine nchini katika mrengo wa upinzani, kupinga pendekezo la kuwepo kwa mazungumzo ya kitaifa, ili kutatua changamoto za vijana wa kizazi cha Gen Z.
Katibu mkuu wa chama hicho Jeremiah Kioni, amesema kuwa wakenya hawana haja ya mazungumzo, kwani tayari wanafahamu matatizo yao, ambayo yamekuwa yakizungumzwa kwenye kila kikao cha mazungumzo ya kitaifa.
Kioni amelalamikia hatua ya vikao hivyo, kutumia fedha nyingi ambazo ni ushuru wa mkenya na kisha baadae serikali kukosa kutekeleza makubaliono ya mazungumzo hayo.
Akizungumzia masuala ya ugumu wa maisha baada ya ongezeko la bei ya mafuta, kioni amesema kuwa serikali, imeongeza bei ya mafuta baada ya msururu wa maandamano ya vijana wa kizazi cha Gen Z, huku akionya wananchi dhidi ya hali ngumu zaidi katika siku za usoni.

