Chama cha DCP kimeitaka tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC, kuwachukulia hatua kali za kisheria, wanasiasa wanaoendeleza semi za kuwa na mipango ya kushiriki wizi wa kura za urais mwaka 2027.
Naibu kinara wa chama hicho Cleophas Malala, amesema kuwa watawasilisha ombi kwa tume hiyo, kuhusiana na suala la kukabili kisheria wanasiasa hao.
Malala amekashifu vikali matamishi hayo, akisema kuwa maamuzi ya wakenya kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2027, hayapaswi kuhujumiwa kwa njia yeyote ile.
Malala amesema kuwa chama hicho, kitakuwa na wagombea wa nafasi mbali mbali za uongozi, katika maeneo ambayo hayana uwakilishi kwenye mabunge ya kaunti, sawa na bunge la kitaifa kwani chama hicho ni cha kitaifa.
Wamezungumza haya wakati wakikaribisha viongozi wapya katika chama hicho, kwenye makao mkuu ya afisi za DCP.

