JAMII KAUNTI YA TANA RIVER YAHANGAISHWA NA NDOVU.

Idara ya KWS tawi la kuanti ya Tana River, imeelezea kuwepo kwa ongezeko la ndovu wanao hangaisha jamii katika maeneo ya Garseni na Tana Delta.

Afisa mkuu wa idara hiyo kaunti ya Tana River, George Bakari amesema kuwa hatua hiyo imechangiwa na mvua kubwa inayoendelea kunya katika maeneo hayo.

Akizungumza na wanahabari, Bakari amesema kuwa hayawani hao, wanatafuta chakula na maji katika maeneo hayo yaliyo na mvua.

Aidha amesema kuwa wapo maafisa wa KWS ambao wanaendelea kushika doria katika maeneo hayo, ili kusaidia katika kuwarejesha Ndovu hao katika mbuga ya wanayamapori ya Tsavo, huku akiwataka wananchi kupiga ripoti kwa maafisa hao pindi watapo ona ndovu hao.