Rais William Ruto ametuma ujumbe wa heri njema kwa jamii ya Waislamu hapa nchini, wanaposherehekea Siku Kuu ya Eid-ul-Adha leo Ijumaa.
kupitia ukurasa wa X, Rais Ruto amewatakia sherehe za amani na furaha tele.
Maadhimisho hayo yanadhihirisha kujitolea kwa mtume Ibrahim, kumtoa mwanawe wa kiume, kama kafara kwa Mungu, kabla ya Mungu kutoa kondoo kuchinjwa kama kafara.
Serikali ya kitaifa mnamo siku ya Jumatano wiki hii, ilitangaza rasmi Ijumaa ya leo, kuwa likizo ya umma, kuadhimisha Eid al-Adha.
Kupitia taarifa maalum kwenye gazeti rasmi la serikali, waziri wa Usalama Kipchumba Murkomen, alitangaza likizo hiyo ili kutoa fursa kwa jamii ya waisilamu, kuadhimisha sherehe hiyo muhimu ya Eid-ul-Adha hii leo.

