SUKARI GHUSHI YENYE THAMANI YA ZAIDI YA SHILINGI MILIONI MOJA YA NASWA KAUNTI YA KWALE.

Maafisa wa Ukusanyaji ushuru Nchini  (KRA) wamenasa lori, lililokuwa likisafirisha magunia 144 ya  sukari, kwa njia haramu, katika mpaka wa Lunga Lunga kaunti ya Kwale.

Baada ya kupokea habari za kijasusi, maafisa wa forodha walisimamisha lori hilo lenye nambari za usajili za kigeni na kupata sukari ambayo haikuwa imekaguliwa.

Lori hilo Lilipopekuliwa kwa kina, magunia 144 ya sukari ya magendo yalipatikana, yakiwa yamefichwa chini ya machungwa, ili kuepuka kulipia ushuru.

Sukari hiyo inakisiwa kuwa thamani ya shilingi 1,080,000.

Kamishna wa forodha na shughuli za mpakani Dkt. Lillian Nyawanda, amesema hatua hiyo ni mojawepo wa juhudi za kukabiliana na biashara ya magendo, katika mipaka ya taifa hili.

Nyawanda amethibitisha kuwa dereva wa lori hilo, hakuwa na stakabadhi zozote husika na usafirisha, sawa na uhalali wa sukari hiyo.

Lori hilo pamoja na sukari hiyo, zinazuiliwa huku uchunguzi wa asasi mbali mbali ukiendelea.