RAILA ODINGA AAHIDI KUSAIDIA JAMII YA KWALE KUPATA HAKI DHIDI YA MZOZO WA ARDHI YA MSIKITI CONGO.

Kinara wa ODM, Raila Odinga sasa anatisha kuwasilisha kesi mahakamani kuhusu utata uliogubika msikiti wa Congo kule kaunti ya Kwale.

Raila aliyezuru eneo hilo, amekashifu mipango ya baadhi ya watu aliowataja kuwa matapeli kujaribu kuinyakua ardhi hiyo ya ekari 16, iliyo na msikiti wa jadi wa Congo.

Raila amesema alitenga ardhi hiyo alipokuwa Waziri Mkuu huku akiahidi kuitetea jamii ya Kwale Islamic Centre kwa hali na mali kuhakikisha inapata haki dhidi ya ardhi hiyo.

Akizungumza na jamii katika eneo hilo, Odinga amenyooshea kidole cha lawama idara ya mahakama kwa madai ya kuendeleza ufisadi katika suala hilo.