ASKOFU MKUU WA KATOLIKI ENEO LA PWANI MARTIN KIVUVA AKASHIFU HATUA YA SERIKALI KUCHUKUA MIKOPO.

Askofu Mkuu wa Dayosisi ya Mombasa Martin Kivuva ameelezea wasiwasi wa kenya kushindwa kulipa madeni yake kwa mataifa na mashirika yaliyo toa mikopo kwa taifa hili.

Kulingana na Askofu Kivuva, deni la kenya kwa sasa limepita kipimo cha kawaida na hivyo serikali ya kitaifa, inapaswa kweka mpango wa kusitisha shughuli za kuchukua mikopo.

Akizungumza katika kaunti ya Mombasa, Kivuva amesema hatua ya serikali ya Rais William Ruto kuendelea kukopa, inaongezea wakenya mzigo mkubwa wakenya kwani watalazimika kulipa madeni hayo kupitia ushuru.

Aidha Askofu Kivuva amemsuta Rais William Ruto kwa kukosa kufuata ushauri anaopewa na wataalamu wengine wa masuala ya kiuchumi, kuhusiana na  mikopo ya kenya.