RAIS WILLIAM RUTO AENDELEA KUWASUTA WAPINZANI WAKE MLIMA KENYA.

Rais William Ruto amewasuta baadhi ya wapinzani wake katika eneo la Mlima Kenya, kwa madai ya kutaka kuwagawanya wakenya kwa misingi ya ukabila.

Kiongozi wa taifa amewaonya wakenya dhidi ya kuhadaiwa na viongozi na kukubali kushiriki siasa za migawanyiko, kwani zitachangia katika kulemaza maendeleo kwa jamii.

Akizungumza katika eneo la Mbeere kaunti ya Embu, Rais amewataka wakenya pamoja na viongozi wa kisaiasa, kutekeleza wajibu wao kwa wananchi walio wachagua.

Kauli yake imeungwa mkono na naibu wake Profesa Kithure Kindiki, ambaye amesema kuwa serikali ya Kenya kwanza, haina mda wa kushiriki siasa za migawanyiko kwa misingi ya ukabila humu nchini.