Maafisa wa polisi eneo Diani kaunti ya Kwale, wamefanikiwa kuwakamata washukiwa 9 wa uhalifu, wanaowahangaisha wenyeji kwa kuwakata mapanga na kuwapora mali zao katika maeneo ya Diani na Ukunda kaunti hiyo.
Tisa hao waliokuwa wamejihami kwa silaha, wametiwa mbaroni usiku wa kuamkia leo, katika maeneo tofauti huko Diani, nakufikisha idadi ya wahalifu waliokamatawa tangu oparesheni hiyo ilipoanza kuwa 145.
Naibu kamanda wa polisi eneo la Msambweni kaunti ya Kwale, Robinson Lang’at amesema kuwa msako huo utaendelea ili kuhakikisha mji wa Diani na viunga vyake, unapata usalama wa kutosha .
Hata hivyo amewataka wazazi kuchunguza miendo ya watoto wao, msimu huu wa likizo huku akiwahakikishia wanyeji na wageni usalama wa kutosha.
Silaha zilizo naswa ni pamoja na mapanga 11, slasher 5, visu 4 ,simu 5, bangi miongoni mwa vifaa vyenginevyo.

