VIONGOZI WA UPINZANI HAPA NCHINI WAKOSOA ZOEZI LA KUWAPIGA MSASA MAKAMISHNA WA IEBC.

Viongozi wanaopinga serikali ya Rais William Ruto wamekashifu vikali jinsi ambavyo zoezi la kuwapiga msasa makamishana wa tume ya IEBC limekuwa likiendelezwa.

Wakiongozwa na kinara wa chama cha Wiper Kalonzo Musyoka, wamesema kuwa viongozi wa kisiasa katika mrengo wa upinzani, wanapaswa kuhusishwa kiukamilifu katika zoezi hilo.

Wakizungumza katika kikao na waandishi wa habari, wamesema kamwe hawatasalia kimya na kuendelea kutizama serikali ikikiuka sheria za taifa hili, hasa katika masuala ya uteuzi wa maafisa wa IEBC.

Kauli yake imeungwa mkono na kinara wa chama cha PNP, Martha Karua ambaye amesema kuwa makamishna, watakao teuliwa kuhudumu kwenye tume hiyo ni wale watakao pendelewa na rais William Ruto na sio kuwa eti wamekubaliwa na wakenya kikatiba.

Kwa upande wake kiongozi wa chama cha DAP-K, Eugene Wamalwa  amemkashifu Raila Odinga kwa kutokuwa na msimamo katika masuala ya siasa, baada yake kujiunga na serikali ya William Ruto.