WAZIRI ADEN DUALE AKABIDHIWA RASMI WIZARA YA AFYA.

Waziri mpya wa afya Aden Duale, ameahidi kukabiliana na walaghai katika wizara hiyo na kuboresha huduma za afya kwa wakenya wote.

Duale ambaye amekabidhiwa rasmi afisi hiyo na mtangulizi wake Dktri Debora Barassa, amesema kuwa sharti wakenya wapate huduma bora kwenye taasisi za afya humu nchini.

Akizungumza katika hafla hiyo, wakati wahudumu wa afya UHC wakiendeleza mgomo wao inje ya afisi za wizara ya afya, kiongozi huyo ameahidi kutatua mzozo wa malipo ya bima ya awali ya NHIF, kwa hospitali za kibinafsi humu nchini.

Kwa upande wake waziri anayeondoka kwenye wizara hiyo Debora Barassa, amejipiga kifua kwa madai ya kuchangia idadi kubwa ya wakenya, kuwa na imani na mamlaka ya SHA, kwa kila alichosema kufikia sasa asilimia 163 zaidi, ya wakenya wamejisajili kwenye bima hiyo.