RAIS RUTO AWATAKA WAPINZANI WAPI KUUZA SERA ZAO KWA WANANCHI.

Rais William Ruto ameonya baadhi ya wapinzani wake dhidi ya kuendeleza kampeni za kukashifu uongozi wake.

Kulingana na Ruto, baadhi ya wapinzani wake wamekosa sera maalum za kushawishi wananchi wa taifa hili, kuwapigia kura katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2027.

Akizungumza katika siku ya kwanza ya ziara yake kule kaunti ya Laikipya, katika eneo la Malima Kenya, Ruto amesema kuwa wakenya, wanadai kusikia mikakati ya viongozi kuhusiana na jinsi watakavyo tatua changamoto zao na sio siasa za kupinga serikali yake.

Vile vile kiongozi wa taifa, amewaisistiza wanasiasa waliochaguliwa kwenye nafasi mbali mbali za uongozi, kutekeleza majukumu yao pasi na kuzungumza kinyume cha viongozi wengine.