Rais William Ruto amemkashifu hadharani waziri wa utumishi wa umma nchini Justine Muturi, kwa kuwa mlegevu katika utendakazi wake, wakati alipokuwa akihudumu katika wadhifa wa mwanasheria mkuu kwenye serikali yake.
Kulingana na Ruto, Muturi alikosa kutekeleza wajibu wake katika kufanikisha ombi la kubuniwa kwa wakfu wa jamii ya waumini wa dini ya kiislamu nchini.
Akizungumza katika hafla ya Ifutar, kwenye ikulu ya Nairobi, Rais Ruto ameihidi kutekeleza ombi hilo, kupitia afisi ya mwanasheria mkuu wa sasa, Dorcas Oduor.
Katika siku za hivi majuzi, waziri Muturi amekuwa akigonga vichwa vya habari kutokana na hatua yake kuwajibisha serikali ya kitaifa katika masuala mbali mbali jambo ambalo limechangia shikizo nyingi kutoka kwa baadhi ya wabunge za kumtaka Muturi kujiuzulu.
Aidha Muturi pia amemjibu rais Ruto na kusema kuwa ombi la waumini hao ni kinyume cha sheria.

