Waziri wa usalama wa ndani Kipchumba Murkomen amesema kuwa serikali ya kitaifa inajitahidi katika kufanikisha suala utumizi wa teknolojia, kwenye idara ya polisi nchini.
Murkomen amesema kuwa utumizi wa teknolojia ya mitandao mbali mbali kwenye idara hiyo, kutarahisishia shughuli za maafisa wa usalama kuhudumia wakenya.
Akizungumza katika kikao na wanadau wa idara hiyo, waziri Murkomen amesema kuwa pia itasaidia pakubwa, kukabiliana na visa vya ufisadi vinavyo endelezwa na maafisa wa polisi katika wizara hiyo.
Vile vile ameongeza kuwa idara hiyo, inaendeleza mikakati ya kuwapatia maafisa wa polisi kamera za siri, sawa na kubuni shughuli za utoaji wa faini pindi tu, mtu atakapo kamatwa, kinyume na ilivyo kwa sasa, ambapo sharti afikishwe kwenye kituo cha polisi.

