HOSPITALI ZA KIBINAFSI NCHINI ZIMEONYWA DHIDI YA KUSUSIA UTUMIZI WA SHA.

Wizara ya afya nchini imewaonya wamiliki wa hospitali za kibinafsi dhidi ya kutotoa huduma za matibabu kwa wananchi, wanaotumia bima ya mamlaka ya SHA.

Katibu wa huduma za matibabu kwenye wizara hiyo Harry Kimutai, amesema kuwa serikali bado imeshikilia msimamo wake, wa kulipa madeni bima ya awali ya NHIF kwa hospitali hizo.

Kimtai aidha ametishia kuwa huenda serikali kuu ikatupilia mbali leseni za hospitali hizo, iwapo zitakosa kutoa huduma za matibabu kwa wananchi kupitia bima mpya ya SHIF.

Kimtai amesisitiza haja ya hospitali na vituo vya afya nchini, kutumia mfumo wa kidijitali ili kuweka wazi aina ya huduma za matibabu na gharama hitajika kwa wagojwa wanao tafuta huduma hizo.

Kwa upande wake mshauri wa masuala ya uchumi katika afisi ya Rais Moses Kuria, amesisitiza kuwa wakenya wanaotafuta huduma za matibabu kwenye hospitali za umma, hawapaswi kutozwa fedha zozote.