WALIMU WAKUU WATAKIWA KURUDISHA VYETI VYA WANAFUNZI.

Waziri wa Elimu Julius Ogamba Migosi, ametoa ilani ya siku kumi na nne, kwa shule zote nchini, kuwapatia wanafunzi vyeti vyao, ambavyo vimezuilia na usimamizi wa shule walizosomea, kutokana na hatua yao kuwa na deni la karo.

Kulingana na Ogamba, ni kinyume cha sheria kwa taasisi za elimu kukosa kuwapatia wanafunzi vyeti vyao, kutokana na ukosefu wa fedha za kulipa madeni ya karo zao na huenda serikali ya kitaifa ikachulia taasisi hizo za elimu hatua kali za kisheria.

Amesema kuwa wizara ya elimu, itashirikiana na tume ya kuajiri walimu katika kuhakikisha kuwa inawakabili walimu wakuu wanao kiuka sheria hiyo.

Aidha baadhi ya wazazi wameendelea kulalamikia suala la wanao kukosa kuendeleza masomo ama hata kupata nafasi za ajira kutokana na ukosefu wav yeti hivyo muhimu.