Wizara ya mambo ya kigeni nchini imebaini kuwa ziadi ya wakenya elfu moja wamefungwa katika mataifa mbali mbali Ng’’ambo na Ughaibuni kufutia ukiukaji wa sheria za mataifa hayo.
Akitoa taarifa hiyo, waziri wa mambo ya kigeni ambaye pia ni mkuu wa maziri nchini Musalia Mudavadi, amewaonya wakenya wanao safiri mataifa hayo dhidi ya kutozingatia sheria za mataifa hayo.
Akirejelea kisa cha Magaret Ndutaa, mkenya mwenye umri wa miaka 37, aliyepewa hukumu ya kunyongwa katika taifa la Vietnam, Mnamo tarehe 6 mwezi huu wa Machi mwaka huu 2025, Mudavadi ameelezea kuwepo kwa ugumu wa kutatuliwa kwa kesi hiyo licha ya wizara yake kuingilia kati.
Akizungumza baada ya kukutana na waziri wa mambo ya kigeni katika taifa la Netherlands, Caspar Veldkamp amesema ameonya wakenya hao dhidi ya kuharibia sifa taifa hili wanapokuwa Ughaibuni ama nchini za Ng’ambo.

