Waziri wa mazingira, Aden Duale na mwenzake wa madini na uchumi wa bahari na maziwa nchini Ali Hassan Joho, wamepongeza hatua ya rais William Ruto kuondoa sheria ya wakenya wa eneo la Kaskazini Mashariki mwa taifa hili kupigwa msasa wanapotafuta vitambulisho vya kitaifa.
Viongozi hao Aidha wamewasuta baadhi ya wale wanaopinga hatua hiyo huku wakitoa wito kwa maafisa wa idara ya usalama kujukumikia wajibu wao katika kufanikisha agizo hilo la rais William Ruto.
Wamesema hatua hiyo italeta afueni kwa wananchi katika jamii za maeneo hayo, ambao pia ni wakaazi wa Ukanda huu wa Pwani.
Kwa upande wake gavana wa kaunti ya Mombasa, Abdulswamaad Shariff Nassir amesema kuwa serikali ya kaunti hiyo, itachukua hatua ya kuendeleza zoezi la kuwasajili wananchi wake kupata stakabadhi hizo muhimu baada ya kukamilika kwa mwezi wa ramadhani.

