Aliyekuwa naibu wa Rais Rigathi Gachagua, ameibua madai ya serikali ya Rais William Ruto kuuza ukumbi wa Bomas jijini Nairobi na mashamba ya magereza yote humu nchini.
Kulingana na Gachagwa, hatua hiyo imefanikishwa baada yake kubanduliwa mamlakani, akidai kuwa kwa sasa hakuna kiongozi anayepinga matakwa ya rais Ruto, kwenye baraza la mawaziri.
Gachangwa ametaja viongozi walio kwenye baraza la mawaziri kuwa wenye uoga na wanaokubaliana na kila kauli ya rais, licha yake kuwa na madhara kwa wakenya.
Gachagwa ametishia kuwepo kwa maovu, anayodai yatatekeleza na serikali ya Rais William Ruto, kwa kile alichosema hakuna viongozi wa kumkosoa kwenye baraza lake la mawaziri.
Aidha, Gachagwa amesema kuwa viongozi wa upinzani, tayari wamepokea maoni ya wakenya na wanaendeleza mikakati ya kubuni sera zitakazo saidia taifa kuboreka kimaendeleo.

