VIWANGO VYA ELIMU VYA DORORA ENEO BUNGE LA MAGARINI KAUNTI YA KILIFI.

Viwango vya elimu katika eneo bunge la Magarini kaunti ya Kilifi vimeripotiwa kudoroa mno, kutokana na hali ya ukame inayoshuhudiwa eneo hilo na kusababisha maisha kuwa magumu, kutokana kuzoroteka kwa kiuchumi.

Kulingana na chifu wa eneo la Marafa, Johnson Mlewa Karena, idadi ya wasomi katika eneo hilo ni kidogo mno, hali ambayo anasema imesababishwa na kuathirika kwa sekta ya kilimo, inayotegemewa sana na wengi wa wakaazi wa sehemu hiyo.

Karema anasema hali hiyo, imechangia ongezeko la familia zisizojiweza katika eneo bunge la Magarini huku asilimia ndogo ya wakaazi, wakipata elimu ya kuwawezesha kupata ajira za kudumu gharama ya maisha.

Wakati huo huo chifu huyo, amesistiza haja ya kuboreshwa kwa maeneo yaliyo na uwezo wa kutoa ajira kwa wakaazi wa Magarini, ikiwemo kivutio cha kitalii cha Hells Kitchen, kilichoko wadi Marafa.