Waziri wa madini na uchumi wa bahari na maziwa nchini Hassan Joho, ametoa agizo la kuondolewa kwa mabwenyenye walionyakua ardhi za fuo za bahari kaunti ya Kwale, kwani walikiuka cha sheria za umiliki wa ardhi.
Waziri Joho amezitaka afisi za kamishna wa Kwale, wizara ya ardhi ,shirika la KWS na ile ya mazingira NEMA, kutumia sheria zilizopo, kuwafurusha mabwenyenye waliojenga katika ardhi za ufuoni, ili kutoa nafasi kwa wavuvi kufanikisha shughuli zao za kiuchumi.
Wakati uohuo ameitaja kaunti ya Kwale kufaidika na miradi mikubwa ya maendeleo kutoka kwa serikali ya kitaifa.
Waziri Joho ameyasema haya wakati wa kuzindua ujenzi wa mradi wa jumba la kisasa, la kuhifadhi samaki almaarufu Mwaepe fishing landing site huko Msambweni kaunti ya Kwale, ujenzi unaofadhiliwa na benki kuu ya dunia, kwa gharama ya shilingi milioni 256.

