WANANCHI KAUNTI YA KILIFI WATAKIWA KUTUMIA NJIA MBADALA KATIKA KUTATUA KESI ZA ARDHI KANDO NA MAHAKAMA.

Waziri wa Ardhi kaunti ya Kilifi, Jane Kamto amewataka wananchi kutokubali kuondolewa kwenye ardhi ambayo, wamekuwa wakiishi kwa zaidi ya miaka kumi na miwili.

Kwa mujibu wa waziri Kamto, kuna haja ya uchunguzi wa mizozo ya ardhi kaunti ya Kilifi kufanywa, ili kusaidia katika kuwalinda wananchi dhidi ya kudhulumiwa na mabwenyenye.

Akizungumza katika wadi ya Ganda eneo bunge la Malindi kaunti ya Kilifi, Jane amewataka wananchi kukumbatia njia mbadala za kusuluhisha mizozo ya ardhi, kando na kuwasilisha kesi hizo mahakamani.

Vile vile amezitaka afisi na mashirika ya kijamii yanayo husika na masuala ya ardhi kaunti ya Kilifi, kuchukua hatua ya kuwasilisha stakabadhi muhimu zinazoweza kutatua mizozo ya ardhi kaunti hii kwa haraka.