RAIS WILLIAM RUTO AAHIDI KUTATUA MIZOZO YA ARDHI KAUNTI YA KILIFI.

Rais William Ruto amehidi kutatua changamoto za ukosefu wa vyeti vya umiliki wa ardhi katika eneo bunge la Magarini kaunti ya Kilifi na Pwani kwa Jumla.

Akizungumza katika wadi ya Sabaki eneo bunge hilo la Magarini, Rais Ruto amesema kuwa tayari serikali kuu, imetenga fedha za kununua ardhi ili wananchi wapimiwe na kupewa hatimili za ardhi hizo.

Aidha Rais amesema kuwa serikali yake, inashirikiana na viongozi wakuu serikalini, ambao pia ni wakaazi wa eneo hili la Pwani ili kutatua changamoto hiyo.

Kwa upande wake gavana wa kaunti ya Kilifi Gideon Maitha Mung’aro amesisitiza haja ya kutatuliwa Cha mzozo wa shamba la ADC.