BULLS YAMSAINI TUVA

Sajili mpya ya klabu ya Young Bulls FC nazungumzia Bruno Tuva kutoka Kathama FC aliisaidia waajiri wake wapya kusajili angalau alama moja nyumbani katika uwanja wa Alaskan jana.

Katika kipindi cha pili Tuva alipata nafasi ya kuingia kambani na kusawazisha bao lililokuwa limefungwa kipindi cha kwanza na Equity na kuwafanya Bulls kuondoa uwanjani hapo na alama.

Tuva ni kati ya maingizo mapya kwenye kikosi cha Young Bulls huku klabu hiyo ikizidisha mawindo ya kunasa sajili mpya kwa ajili ya kuisaidia Young Bulls kutoshuka daraja kutoka daraja la kwanza.

Kwa sasa Young Bulls inayoongozwa na kocha Jackson Kalinga inashikilia mkia katika ligi hiyo baada ya kuanza msimu huu vibaya kwa changamoto za ndani na nje ya uwanja ambazo pia zachangiwa na masuala ya uchumi.