Viongozi wa Pwani katika bunge la kitaifa na lile la Seneti nchini, wamemtaka rais William Ruto kuteua mmoja wao, kuwa mwenyekiti wa kamati ya bajeti kwenye bunge la kitaifa.
Wakiongozwa na seneta mteule Mirajj Abdullahi na mbunge wa Matuga kaunti ya Kwale, Kassim Sawa Tandaza, wametaja suala la rasilimali za Pwani, kuwa na mchango mkubwa katika uchumi wa taifa, kama mojawapo ya sababu zao kuadai nafasi hiyo ya uongozi.
Wakizungumza na waandishi wa habari kaunti hiyo, wakati ambapo rais William Ruto, anatarajiwa kuzuru kaunti mbali mbali za Pwani, viongozi hao wamelalamikia suala la ukabila, kuendekelezwa katika bunge hilo kwenye uteuzi wa viongozi wa kamati mbali mbali.
Kwa upande wake mbunge wa Garsen kaunti ya Tana River, Ali Wario amesema kuwa hatua hiyo, itaimarisha pakubwa uhusiano kati ya Rais William Ruto na viongozi wa kisiasa eneo la Pwani.
Kuali hizo zinajiri baada ya kushuhudiwa kwa msukosuko wa uongozi wa kamati mbali mbali kwenye bunge la Kitaifa.

